budget

wakati bunge linaendelea kijadili budget inaelekea wabunge wa ccm wamepitwa na wakati na kushidwa kutetea na kuelezea kwanini budget ni nzuri kwa watanzania. wabunge wapinzani kwa upande wao wemeonyesha muelekeo nzuri wa kuhoji budget kwa hoja nzito na za maana. another silly season, business as usual, copy and paste budget nothing new, budget isiyo tekelezeka..etc.

Haya ni maneno makari  na kwa siri-kali makini inabidi iyachukue na kuyatafakari kwa makini. itakuwa hatari kwa siri-kari ya ccm kupuza kilio cha watanzania kupitia wabunge wao wapinzani na kujidai business as usual.  maisha ya watanzania ni magumu; maji tabu, umeme unakatika katika kama disco lights, hospitali hoi, wanafunzi wanafail, hatuna ndege za uhakika, raili ya kati hoi, tazara tunawaita wachina tena kutusave, barabara mbovu na mengine mengi nitachukua siku nzima na ukurasa hu wote kuorothesha yote.

kuna vizuri pia lakini vibovu vimezidi sana vinanifanya hata machache mazuri kutoyashabikia.

Kupanga ni kuchagua. Mimi binafsi nilihamasika nilipokuwa namsikiliza raisi akizindua mpaango wa kabambe wa maendeleo wa miaka 5. Kupanga sio kutekeleza. Mpango huu ndio uliopaswa kuanza kutekelezwa rasmi budget hii kwa kutenga 35% ya mapato ya ndani kutekeleza mpango huu. Kupanga+Kutekeleza=Results(maendeleo). Kwa mwanzo hu mpango wa miaka 5 siri-kali haiko serious na sio kitu kigeni. mipango mingi mizuri emeishia kwenye mafile tu. nothing new….

Sitaki kuichambua budget yote hapa lakini natoa mfano huu kumake my point clear. Tanzania sisi matajiri sana lakini kwa mwelekeo huu ndio maana tupo maskini sana. Tuna mali nyingi sana lakini kwa umaskini wa mawazo ya watawala wetu ndio tupo hapa miaka 50 ya uhuru. Tunaitaji mapinduzi ya akiri, kijamii na utawala mzima ili tuvune matunda ambayo mwenyezi mungu ametubarikia nayo madini, maziwa, mt kilimanjaro, bahari, mbuga za wanyama, ardhi nzuri na mengineyo. Other wise tuendelee na hii silly seasson

This entry was posted in politics/siasa and tagged , , , , . Bookmark the permalink.

Leave a comment