raisi ni dhaifu

“udhaifu wa raisi” ni tofauti na kusema “Raisi ni dhaifu”. kwa wale wanaojua kiswahili fasaha watanisaidia kwa hili. Labda nibadilishe maneno kidogo ili tuelewane kidogo; “ujinga wa raisi” si sawa na kusema “raisi ni mjinga”. Mimi niko na ndugu Mnyika kwa kusema raisi ni dhaifu na ni kweli ni dhaifu.

Raisi dhaifu ni ambaye ajui kama kwenye baraza lake la mawaziri kuna uozo mpaka bunge llimwambie so. Baada ya kuambiwa anasita sita kuchukua hatua mpaka dakika za mwisho. dhaifu=weak(in politics) means: 1-not having much political strength, governing power, or authority. 2-not strong; liable to yield, break, or collapse under pressure or strain. Fragile.

Tupo kwenye democrasia ambayo inatupa uhuru wa kusungumza na kusema jambo lolote as long as we dont hurt ony1. Ndugu Mnyika yuko sahihi kumwita raisi ni dhaifu lakini kwa kujua sheria za bunge zitambana makusudi akasema UDHAIFU WA RAISI. Kwani anazo haki za kuzungumza kwa uhuru na katiba inampa uhuru huo. Kwa sheria za bunge hakuvunja sheria yoyote kwa sababu hakumwita raisi dhaifu ila alisema udhaifu wa raisi ambanyo ni vitu viwili tofauti kabisa. Angesema raisi ni dhaifu angekuwa amevunja sheria  kwa mtazamo wangu na kustaili kutolewa nje ya bunge.

Speaker, naibu speaker na wasaidizi wao wote waendeshao bunge wawe makini na kutenda haki kwa wabunge wote ccm na wapinzani. WATANZANIA tunawaangalia na historia pia inawatazama kwa jicho kali sana. Hata kwenye vitabu vitakatifu inasemwa utakuja kuhukumiwa kwa mazuri au mabaya unayotenda now. Na hukumu yetu haiko mbali sana kama ya kwenye vitabu vitakatifu ila ni 2015. Ni Karibu sana

Bunge letu limechukua kwa karibu sana mfumo wa bunge la uengereza. Mnamo mwaka 1997 tony blair wakati ni mku wa kambi ya upinzani alimwita waziri mku wa wakati huo john mojor dhaifu(weak, weak, weak). Speaker hakuzui na kumtaka mr blair kuondoa kauli hiyo. Uchaguzi uliofatia mr mojor alishidwa na mr blair alichaguliwa kuwa waziri mku wa uengereza. Huu ni mfano mzuri wa siasa iliyo komaa na fundisho kwa speaker Anna makinda, siri-kali ya ccm, wabunge wote na wanasiasa kwamba mwishoni ni wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho.

This entry was posted in politics/siasa and tagged , , , , , . Bookmark the permalink.

Leave a comment